ACCUEIL » Habari kwa kishwahili » USUMBUFU MPAKANI

USUMBUFU MPAKANI

Watu ambao wanatumiya Barabara ya Kavimvira kuelekeya Bujumbura, wanaendeleya kupata taabu kutokana na maji mengi ambayo hayaruhusu magari madogo madogo kupita kwa usalama.

Maji yanaonekana kuwa mengi kutoka ndani ya Ziwa Tanganyika na Mto Nyangara. Siku zilizo pita, gari nyingi zilihasirika zilipo jaribu kuyavuka maji hayo. Mengi kati ya magari madogo madogo yaliyo jaribu kuvuka mpaka kupitiya maji hayo, yaliingiliwa na maji na kuharibika vikali

Mashirika ya usafiri kama MAPASSA yaliamuwa kubadili namna yao ya kusafirisha wateja wao.

Wateja kutoka Bujumbura na Bukavu wanashushwa pakavu hapo mpakani na kuchukuliwa na mengine magari ya aina ya Land cuiser ambao yanayo uzowefu wa barambara ngumu na kuvushwa upande mwengine ambapo gari zingine zinawasubiriya kwa kuendelesha safari yao.

Kazi za kutengeneza barabara hii ya mpakani Kavimvira , tayari zimeanza zikifanyika na mashirika ya kutengeneza ma barabara kutoka Burundi.

Petit Gabriel de Brigitte

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *

Retourner en haut de la page