ACCUEIL » Habari kwa kishwahili » Afcon 2023: Je, Ivory Coast, Nigeria, Misri, Ghana na Senegal zina nafasi gani katika Kundi A, B na C?

Afcon 2023: Je, Ivory Coast, Nigeria, Misri, Ghana na Senegal zina nafasi gani katika Kundi A, B na C?

footballeurs africains

Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2023 inaanza nchini Ivory Coast katikati ya Januari baada ya kuahirishwa ili kupisha msimu wa mvua Afrika Magharibi.

Huku Senegal ikitazamia kutetea ubingwa wao, muundo wa timu 24 unamaanisha kwamba timu mbili za juu kutoka kila kundi zitafuzu hadi hatua ya mtoano, huku timu nne bora zilizo katika nafasi ya tatu zikiungana nao.

Kulikuwa na mshtuko katika Kombe la Mataifa lililopita nchini Cameroon, huku Comoro na Gambia, mabingwa mara nne Ghana wakirejea nyumbani mapema, lakini tunaweza kutarajia nini kutokana na toleo la 34 la michuano hiyo ya bara?

BBC Sport Africa imezungumza na wachezaji, magwiji wa soka barani Afrika na waandishi wa habari ili kuangazia kundi A, B na C.

(Habari kutoka: BBC News Swahili)

Retourner en haut de la page